Logo
UANACHAMA
...

Membership

UANACHAMA IFM WORKERS SACCOS

Kwa mujibu wa Msingi wa kwanza (1) wa Ushirika kimataifa na Masharti ya chama ibara ya 10, Uanachama wa IFM WORKERS SACCOS uko wazi kwa mtumishi yeyote yule wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Taasisi ya umma au binafsi ili mradi tu awe tayari kufaidika na huduma zake na kufuata Sheria, Kanuni, na Masharti ya IFM WORKERS SACCOS limited. Wanachama ni wale wote waliokuwepo tokea kuanzishwa kwake na wanaoendelea kujiunga kwa mujibu wa masharti ya Chama

SIFA ZA KUJIUNGA IFM WORKERS SACCOS

Ili uweze kuwa mwanachama wa IFM WORKERS SACCOS na kupata faida mbalimbali ambazo mwanachama anafaidika nazo lazima uwe na sifa zifuatazo;

  1. Uwe mwajiriwa wa Taasisi ya umma au binafsi
  2. Kujaza fomu ya uanachama
  3. Kulipa kiingilio cha Sh. 100,000
  4. Kuchangia akiba ya 7% ya kipato chako kila mwezi
  5. Kulipa hisa kila mwezi (kima cha chini Sh. 10,000)
  6. Kuchangia michango ya mwezi kupitia mshahara
  7. Kuitambulisha IFM WORKERS SACCOS Ltd kwa mwajiri
  8. Huduma zingine zitatolewa kwa kuzingatia vigezo na masharti ya huduma husika

FAIDA ZA KUJIUNGA NA IFM WORKERS SACCOS

Katika ubunifu wa mazao ya bidhaa za kifedha na Huduma kwa wanachama na wadau wa IFM WORKERS SACCOS wanafaidika na;

  1. Viwango vya riba vya mikopo ambavyo ni shindani na nafuu.
  2. Mapato ya kuvutia kwa wanachama wanaowekeza fedha zao kupitia Akiba, Amana, na Akiba Maalum.
  3. Uchaguzi mpana wa bidhaa za kifedha, hususan mikopo.
  4. Uwazi wa gharama katika miamala ya uchukuaji wa Amana na Akiba Maalum.
  5. Malipo ya gawio kwa wanahisa pamoja na riba kwenye Akiba na Amana.
  6. Ulinzi dhidi ya majanga yanayoweza kuathiri mikopo.
  7. Nafasi ya kushiriki majadiliano kuhusu uwekezaji wa fedha zao.

WAJIBU WA MWANACHAMA WA IFM WORKERS SACCOS

Kila mwanachama anaowajibu katika chima, Yafuatayo ni wajibu wa kila mwanachama wa IFM WORKERS SACCOS

  1. Kukamilisha kununua hisa na kuweka akiba kwa kuzingatia Masharti sera na miongozo iliyopo katika chama.
  2. Kufuata na kutekeleza Sera, Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama, maazimio ya Mikutano mikuu na maelekezo mengine halali kwa mujibu wa Sheria za nchi;
  3. Kurejesha mkopo kwa kufuata mkataba wa mkopo;
  4. Kutoa michango mbalimbali katika kuendeleza madhumuni ya chama kadri itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu;
  5. Kubeba dhamana endapo janga lolote litakipata chama;
  6. Kuwa mwaminifu na kuonesha ushirikiano katika kutekeleza shughuli za chama;
  7. Kumdhamini mkopo mwanachama mwenzake isipokuwa mwanachama aliyedhamini hatakuwa na haki yakudhaminiwa na mwanachama aliyemdhamini katika kipindi kile kile;
  8. Kuhudhuria semina na mafunzo yanayotolewa na IFM WORKERS SACCOS katika mpango wake wa elimu na mafunzo mengine yatakayotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika au wadau wa kisekta

HAKI ZA MWANACHAMA WA IFM WORKERS SACCOS

Kila mwanachama ana haki katika chama sawa na mwanachama mwengine, zifuatazo ni haki za kila mwanachama wa IFM WORKERS SACCOS

  1. Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano yote inayohusika;
  2. Kushiriki katika kutoa uamuzi wa mambo mbalimbali katika Mikutano Mikuu;
  3. Kupiga kura chini ya misingi ya mtu mmoja kura moja bila kujali idadi ya Hisa anazomiliki;
  4. Kuchagua na/au kuchaguliwa katika Uongozi wa chama.
  5. Kuwa na haki sawa kuhusu mali ya Chama na kudhibiti ipasavyo matumizi yake;
  6. Kupatiwa huduma zozote zinazotolewa na chama ilimradi amekidhi masharti yanayoambatana na huduma hiyo;
  7. Kupatiwa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za IFM WORKERS SACCOS, muhtasari wa mkutano na nyaraka nyingine za chama kwa ajili ya mapitio akiwa katika ofisi za chama;
  8. Kuteua Mrithi;
  9. Kupokea gawio na faida nyingine kutoka katika shughuli za chama kwa kuzingatia masharti; na
  10. Kupewa kitabu cha Akiba au kifaa kingine chenye makusudi hayo.

IFM WORKERS SACCOS

5 Shaaban Robert Street, Dar es salaam Tanzania

Phone: +255 756 123456

Email: ifmworkerssaccos@gmail.com

KURASA ZA KARIBU

Nyumbani

Kuhusu Sisi

Huduma Zetu

Nyaraka

Mawasiliano

HUDUMA ZETU

Mikopo ya Maendeleo

Mikopo ya Dharura

Mikopo ya Papo Kwa Papo

Mikopo ya Weekend

Mikopo ya Mishahara

TUNAPATIKA

Dar es salaam

Dodoma

Mwanza

Simiyu

© Copyright IFM WORKERS SACCOS. All Rights Reserved